radi wetu unafanyakazi na wahamiaji na wakimbizi Queensland kote ili kuboresha habari za magonjwa ya Ini, VVU/UKIMWI na afya ya kijinsia. vipimo na huduma za utibabu.
Mradi wetu unafadhiliwa na Wizara ya Afya ya Queensland. Huduma na rasilimali zetu zote zinatolewa bure kwa wahamiaji na wakimbizi wote pamoja na watu wasio na kadi ya Medicare na watoa huduma wanao fanya kazi na watu hao.
Elimu ya jamii na utoaji wa habari
Timu yetu ya wafanyakazi wa afya ya jamii waliopewa mafunzo ya lugha zaidi ya mbili (BCHWs) hutoa elimu kwa lugha nyingi kwa vikundi vya jamii kote Queensland. Pia tunatoa habari kupitia njia ya simu, mitandao ya kijamii (kama vile Facebook,WeChat,WhatsApp), magazeti ya kikabila na redio kwa kiingereza na lugha nyingine.
Kuomba kipindi cha elimu cha bure kwa kikundi chako tafadhali bonyeza hapa.
Kuomba habari kwa lugha yako tafadhali wasiliana na wafanyakazi wetu wa lugha zaidi ya mbili hapa chini.
Msaada
Timu yetu hutoa msaada wa kibinafsi na habari kwa watu wanaoishi na magonjwa ya ini na kwa familia zao, kwa mfano:
- Kusoma na kuelezea/tafisiri barua kutoka kwa Mganga wako au Hospitali
- Kufanya miadi ya matibabu
- Kukuonyesha jinsi ya kufika Hospitalini ikiwa ni mara yako ya kwanza kwenda kwa Mganga wako
- Kukusaidia kuwasiliana na Mganga wako au H
Kwa maelezo zaidi ya jinsi tunavyoweza kukusaidia wewe na familia yako tafadhali wasiliana na Meneja wa Mradi kupitia health@eccq.com.au au simu 38449166. Vinginevyo, unaweza kuwasiliana na mmoja wa wafanyakazi wetu wa lugha zaidi ya mbili wanao ongea lugha yako kwa njia ya simu au barua pepe kama ilivyo hapo chini.
Kuomba msaada wetu tafadhali bonyeza hapa
Kipimo cha fibroscan
Fibroscan ni kipimo salama, cha haraka na kisicho na madhara cha kutathimini uwezekano wa uharibifu kwenye ini. Huduma hii ni bure kwa watu wenye magonjwa ya ini B au C. Utahitaji uwe na barua ya rufaa kutoka kwa Mganga wako kufanya fibroscan. Kwa habari zaidi juu ya huduma yetu ya fibroscan tafadhali wasiliana na Mratibu wa Matibabu na Usimamizi kwa referrals@eccq.com.au au 38449166.
Kuomba fibroscan tafadhali bonyeza hapa ( lazima iwe imekamilishwa na Mganga wako).







