BBV Swahili

radi wetu unafanyakazi na wahamiaji na wakimbizi Queensland kote ili kuboresha habari za magonjwa ya Ini, VVU/UKIMWI na afya ya kijinsia. vipimo na huduma za utibabu.

Mradi wetu unafadhiliwa na Wizara ya Afya ya Queensland. Huduma na rasilimali zetu zote zinatolewa bure kwa wahamiaji na wakimbizi wote pamoja na watu wasio na kadi ya Medicare na watoa huduma wanao fanya kazi na watu hao.

Elimu ya jamii na utoaji wa habari

Timu yetu ya wafanyakazi wa afya ya jamii waliopewa mafunzo ya lugha zaidi ya mbili (BCHWs) hutoa elimu kwa lugha nyingi kwa vikundi vya jamii kote Queensland. Pia tunatoa habari kupitia njia ya simu, mitandao ya kijamii (kama vile Facebook,WeChat,WhatsApp), magazeti ya kikabila na redio kwa kiingereza na lugha nyingine.

Kuomba kipindi cha elimu cha bure kwa kikundi chako tafadhali bonyeza hapa.

Kuomba habari kwa lugha yako tafadhali wasiliana na wafanyakazi wetu wa lugha zaidi ya mbili hapa chini.

Msaada

Timu yetu hutoa msaada wa kibinafsi na habari kwa watu wanaoishi na magonjwa ya ini na kwa familia zao, kwa mfano:

  • Kusoma na kuelezea/tafisiri barua kutoka kwa Mganga wako au Hospitali
  • Kufanya miadi ya matibabu
  • Kukuonyesha jinsi ya kufika Hospitalini ikiwa ni mara yako ya kwanza kwenda kwa Mganga wako
  • Kukusaidia kuwasiliana na Mganga wako au H

Kwa maelezo zaidi ya jinsi tunavyoweza kukusaidia wewe na familia yako tafadhali wasiliana na Meneja wa Mradi kupitia health@eccq.com.au au simu 38449166. Vinginevyo, unaweza kuwasiliana na mmoja wa wafanyakazi wetu wa lugha zaidi ya mbili wanao ongea lugha yako kwa njia ya simu au barua pepe kama ilivyo hapo chini.

Kuomba msaada wetu tafadhali bonyeza hapa

Kipimo cha fibroscan

Fibroscan ni kipimo salama, cha haraka na kisicho na madhara cha kutathimini uwezekano wa uharibifu kwenye ini. Huduma hii ni bure kwa watu wenye magonjwa ya ini B au C. Utahitaji uwe na barua ya rufaa kutoka kwa Mganga wako kufanya fibroscan. Kwa habari zaidi juu ya huduma yetu ya fibroscan tafadhali wasiliana na Mratibu wa Matibabu na Usimamizi kwa referrals@eccq.com.au au  38449166.

Kuomba fibroscan tafadhali bonyeza hapa ( lazima iwe imekamilishwa na Mganga wako).

Rasilimali

Rasilimali zilizo chapishwa: tume andaa rasilimali lugha mbalimbali zilizo chapishwa kwa magonjwa ya ini B,magonjwa ya ini C ,VVU/Ukimwi, magonjwa ya zinaa na fibroscan. Tafadhali bonyeza hapa kupata rasilimali na bonyeza hapa kupakua fomu ya maagizo.

Okoa Maisha – Kapimwe Ini

Play Video

World AIDS Day 2024

Play Video

Siku ya Hepatitis Duniani

Play Video

Kondomu (Mipira ya kujamiiana) : Tunatoa kondomu za bure na pakiti za sampuli zilizo na saizi tatu za kondomu, hizi zinaweza kutumwa kwako. Unaweza kuagiza kondomu kwa:

Wasiliana na wafanyakazi wetu wa lugha zaidi ya mbili

Jina la wafanyakaziLughaSimuBaruapepe
AngelineKifaransa,Kirundi,Kinyarwanda,kiingereza0481 838 692angelinem@eccq.com.au
ChristineAcholi, Juba Kiarabu, Kiswahili,kiingereza0479 036 383christineo@eccq.com.au
DanielDinka, kiarabu, Juba Kiarabu, kiingereza0479 062 234daniela@eccq.com.au
EvelynKiburma , Kiingereza0481 827 751evelynp@eccq.com.au
IqbalDari, Kiingereza0403 681 929iqbalp@eccq.com.au
LazaroKiswahili, Kirundi, Kiingereza0479 153 742lazarok@eccq.com.au
NellieKichina,Kiingereza0479 130 997

 

3844 6877

chinese@eccq.com.au
TamKivietinamu, Kiingereza0428 223 052

 

3844 3122

vietnamese@eccq.com.au

Maoni/Marejesho?

Ikiwa una mapendekezo yoyote au ungependa kutoa maoni juu ya huduma na rasilimali zetu tafadhali wasiliana na Meneja wa Shirika kupitia health@eccq.com.au au 3844 9166.

Viunga kwa taarifa zaidi

Wizara ya Afya Queensland – www.qld.gov.au/health/staying-healthy/sexual-health

Jumuiya ya Tiba za Ukimwi (ASHM) – www.ashm.org.au

Shirika la True Reelationship – www.ture.org.au

Watu wa Mwangao Mzuri Queensland (QPP) – www.qpp.org.au

Magonjwa ya Ini Queensland – www.hepqld.asn.au

Baraza la UKIMWI la Queensland la mapenzi ya jinsia moja – https://quac.org.au/

Mtandao wa Afya wa Jipigao Sindano Queensland – www.quihn.org

Heshima(Respect) – www.respectqld.org.au

Signup for Multicultural Partners Newsletter